December 29, 2019


ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC, leo anangia kikaangoni tena baada ya kupoteza mechi yake ya pili akiwa kwenye benchi la ufundi ndani ya Azam FC kwa kufungwa bao 1-0 na Coastal Union ya Tanga.

Leo atakutana na timu ya Polisi Tanzania iliyotoka kushinda mabao 2-1 mbele ya KMC uwanja wa Ushirika, Moshi.

Mechi ya kwanza kwa Cioaba ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting ambayo alikuwa ugenini na alifungwa bao 1-0 mchezo wake wa pili kupoteza ilikuwa mbele ya Coastal Union alifungwa pia bao 1-0 uwanja wa Mkwakwani.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa umakini ulikosekana katika kumalizia nafasi za mwisho.

“Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila timu inapambana kupata matokeo ila nina amini tutafanya vizuri kwenye mechi zetu zinazofuata,” amesema Cheche.




1 COMMENTS:

  1. Kocha mlimfukuza leo tena mmemrejesha wachezaji magarasa wameachwa na wenzenu mmeenda kuwaokota nyinyi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic