December 29, 2019



IMEBAINIKA kuwa uongozi wa Polisi Tanzaia umepania kubana matumizi ya usajili kwa kusajili wachezaji ambao wapo huru ili kupunguza gharama za uhamisho kwa mchezaji.

Polisi Tanzania ipo chini ya Kocha Mkuu wa Malale Hamsini ambaye amepewa kandarasi hiyo akichukua mikoba ya Seleman Matola ambaye amejiunga na Simba kwa sasa.

Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa malengo ya Polisi Tanzania ni kufanya usajili mzuri ila usiwe wa gharama jambo lililowafanya waache nyota wengi waliokuwa kwenye hesabu zao msimu huu.

“Kuna wachezaji wengi wazuri ambao wanahitajika na Polisi Tanzania ila kwa sasa hawatasajiliwa kutokana na kukwepa gharama ndio maana wanasajiliwa wale walio huru kama ilivyo kwa Pius Buswita,” alieleza mtoa taarifa.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa wamejipanga kufanya usajili makini ambao wataumudu kwa kuongeza jumla ya wachezaji wanne ambao wanahitajika ndani ya kikosi.

“Tunahitaji kusajili wachezaji wanne ambao tutawamudu na wenye uwezo wa kutosha, kwa sasa tumemalizana na Buswita wengine wanakuja, tumebakiza wachezaji watatu tu kwenye dirisha hili dogo,” amesema Lukwaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic