UONGOZI wa Yanga umeamua kuanza kujipanga kwa ajili ya mzunguko wa pili baada ya leo kumtambulisha nyota mpya kwa mashabiki wao ambaye anakuwa ni nyota wa pili.
Adeyun Ahmad Selemen beki aliyekuwa anakipiga ndani ya JKT Tanzania sasa ni mali halali ya Yanga.
Seleman amesaini mkataba wa miaka miwili itakayomfanya awatumikie wana Jangwani hao wenye maskani yao Kariakoo.
Huyu anakuwa ni mchezaji wa pili kutambulishwa rasmi huku wa kwanza akiwa ni rasta Tariq Seif aliyetoka nchini Misri.
Hiyo timu ina mademu kila kona mpaka wachezaji wa zamani wanadamu,halafu wewe Adayum unasaini.Tafadhali tusikusikie ukilalamika umeyakubali yavumilie
ReplyDeleteHujaeleweka umeandika nini.Mademu kila kona.........wachezaji wa zamani wanadamu.......punguza mihemko
DeleteHahahahaaaaaa..naona upande wa pili mapovu yanawatoka...vp kwani kuna ttz ktk hili?
ReplyDelete