December 18, 2019


MEDDIE Kagere, mshambuliaji nyota wa Simba, amerejea kwao Rwanda na kwa sasa hayupo na kikosi kilicho chini ya Mbelgiji Sven Vanderbroeck ambaye amechukua mikoba ya Patrick Aussems.

Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa iliyomuondoa kikosini Kagere ni matatizo ya kifamilia kwa sasa na amekwenda kuyashughulikia 

Taarifa zinasema Kagere hatakuwa katika kikosi hicho kwa muda kutokana na matatizo hayo ya kifamilia ambapo mama yake mzazi anaumwa hivyo amekwenda kumjulia hali.


Kagere msimu uliopita alikuwa ni kinara wa utupiaji baada ya kufunga jumla ya mabao 23 na kwa sasa ni kinara akiwa ametupia jumla ya mabao nane ndani ya ligi.

3 COMMENTS:

  1. Enter your comment...mada haiendani na kichwa cha habar

    ReplyDelete
  2. Basi hiyo sio kutimka, ni kwenda kumjuulia hali mama yake mgonjwa. Kutimka ni pale mchezaji anapoondoka kwa ugomvi, kwamfano anatimka mchezaji pale anapokuwa halipwi chake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama wale wa kutoka mataifa nje ya Tanzania waliotimka kutoka dimbwini

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic