December 29, 2019


KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solkskjaer amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa nyota wake wanaounyesha kwa sasa ndani ya uwanja.

"Wanaonyesha kitu cha kipekee na ni furaha kwangu na mashabiki kuona wanafanya vile ambavyo tunahitaji," amesema.

United jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burney ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Newcastle United uliochezwa Alhamisi ya Desemba 26, Old Trafford.

Mabao ya United yalifungwa na Anthony Martial dakika ya 44 na Marcus Rashford dakika ya 90+5.


Ushindi huo unaifanya United kuwa nafasi ya tano baada ya kujikusanyia pointi 31 huku Burney ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake 24 na zote zimecheza mechi 20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic