December 29, 2019


 SELEMAN Mataso, Mwenyekiti wa Biashara United amesema kuwa wanawatambua vema Yanga hivyo watapambana kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wao wa kesho wa ligi utakaochezwa uwanja wa Uhuru.

Biashara United itamenyana na Yanga, Desemba 30 ikiwa ni mchezo wao wa 12 ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 15 wapinzani wao Yanga wapo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 10 na wana pointi 21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mataso amesema kuwa wanautambua mfumo wa Yanga jambo ambalo haliwapi shida wana imani watawapa taabu watakapokutana kwenye mechi hiyo.

“Tunatambua kwamba wameshinda mbele ya Tanzania Prisons ila hiyo haiwapi nafasi kututisha nasi kwenye mchezo wetu lazima tutawape taabu na hesabu zetu ni kupata pointi tatu muhimu,” amesema Mataso.


3 COMMENTS:

  1. Sawa endeleeni kuikamia Yanga mwisho kitawakuta kilichowakuta Stand United. KMC: Mbeya City ; Ruvu Shooting wameshangilia kupata matokeo kwa wana wakajiona wamemaliza ligi sasa wanapumulia mashine

    ReplyDelete
  2. Unawatisha wawaachie. Chezeni mpira. Hakuna kushinda kwa jina. Mpira uwanjani.

    ReplyDelete
  3. Maneno mengi ya nini?,goli 2tuu Zina wa subiri mbele yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic