December 18, 2019


Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amewatangazia vita wa Yanga kwa kusema kuwa, wanatumia michezo iliyobaki ya ligi na Kombe la FA kujiwinda dhidi yao.

Matola ambaye ametua Simba hivi karibuni akitokea Polisi Tanzania akishirikiana na kocha mpya wa timu hiyo, Sven Vanden Broeck raia wa Ubelgiji wana kibarua mbele yao cha kuhakikisha wanaifunga Yanga Januari 4, mwakani.

Akizungumza na Spoti Xtra, Matola amesema; “Kabla ya mchezo wetu na Yanga kuna michezo minne ipo mbele ambayo ni dhidi ya Lipuli, KMC na Ndanda kwa upande wa ligi na mchezo wa FA ambayo yote tunahitaji kushinda ili tuweze kujiweka sawa.

“Tunatumia muda huu kukipanga kikosi chetu ili kiweze kuwa bora japokuwa mchezo wa Yanga upo mbali naamini tutakapomaliza mechi hizi ndipo tutaanza kujipanga dhidi ya mchezo huo,” alisema Matola ambaye amewahi kuikochi Lipuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic