Timu ya Mbeya City FC imejikuta kwenye wakati mgumu baada ya viongozi wake wa benchi la ufundi kushambuliwa na mashabiki wa timu ya Migombani FC.
Tukio hilo ambalo lilisababisha viongozi kadhaa kujeruhiwa kwa mawe lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Vwawa mkoani Songwe.
Mashabiki wa Migombani FC walianza vurugu hizo baada ya timu yao kuondolewa kwenye mashindano ya Azam Federation Cup kwa mikwaju ya penalti.
Taarifa iliyotolewa na Mbeya City FC inasema meneja wao ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Mwegane Yeya alipasuliwa kwenye paji la uso, huku kioo cha mbele cha basi la timu hiyo likishambuliwa na kupasuka.
Katika mchezo huo Mbeya City walifanikiwa kupata ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penalti. Hadi tunaingia mitamboni hakuna tamko lolote kutoka kwa mamlaka za soka kuhusu vurugu hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment