UONGOZI wa Polisi Tanzania umesema kuwa bado unamtambua mshambuliaji wao Ditram Nchimbi kuwa ni mali ya Polisi Tanzania licha ya habari kueleza kuwa amemalizana na Yanga.
Nchimbi anayekipiga ndani ya Polisi Tanzania kwa mkopo ni mali halali ya Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na Yanga ambao wanahitaji saini ya Nchimbi.
Msimu huu amekuwa wa kwanza kufunga hat-trick ambapo aliifunga Yanga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa Uhuru na ililazimisha sare ya mabao 3-3 jambo lililomuongezea umaarufu ghafla nyota huyo wa zamani wa Njombe Mji inayoshiriki Daraja la Kwanza kwa sasa.
Frank Lukwaro, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania amesema kuwa bado Nchimbi ni mali yao kwani hawajapata taarifa zozote zile mpaka sasa.
"Hatuna tatizo na Nchimbi kwenda Yanga ila kwa sasa ni mali yetu kwa kuwa tumemchukua kwa mkopo kutoka Azam na bado ni mali yetu ikiwa Yanga wanamhitaji ni lazima wafuate utaratibu," amesema.
Nchimbi kwenye Ligi Kuu Bara ametupia jumla ya mabao manne huku kinara wa kutupia akiwa ni Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 8.
0 COMMENTS:
Post a Comment