UONGOZI wa Yanga upo katika hatua za mwisho za kuweza kuinasa saini ya beki wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto ili kuweza kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
Imeelezwa kuwa benchi la
ufundi la Yanga tayari limeshapitisha jina la beki huyo kuweza kumalizana nae
katika usajili wa dirisha dogo.
“Moja ya majina
ambayo yamekuwa yakijadiliwa katika kikao kilichofanyika Kigoma, Mwamnyeto amekuwa akipewa
kipaumbele baada ya kutokea katika ripoti zote mbili kutoka kwa kamati ya
mashindano na benchi la ufundi chini ya kocha, Boniface Mkwasa.
“Tayari kuna
mazungumzo yanaendela kati ya ungozi na beki huyo kwa ajili ya kuinasa saini
yake iwapo watafikia muafaka,” amesema mtoa taarifa.
Meneja wa Mwamnyeto, Kassa Mussa ameuambia mtandao wa Saleh Jembe kuwa amekuwa akipata ofa nyingi za mteja wake kwa sasa kutokana na uwezo wake.
"Nina ofa nyingi zinamtaka mchezaji wangu kwa sasa tupo kwenye mazungumzo wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi," amesema.

0 COMMENTS:
Post a Comment