December 26, 2019


Nimeona watu wakisema mengi baada ya kutoa zawadi ya viatu vya kisasa kwa kiungo wa Yanga, napenda kumuita Cynthia... Wako wamesema apewe shukurani Haji Manara
Nafikiri ni maoni yao lakini anayemdhihaki mtu, halafu wengine wakampa moyo, ukiona ndiye anapaswa kupewa shukurani sawa, kila mtu ana mawazo yake TUYAHESHIMU.

Namfahamu huyu binti kitambo na nimesafiri na Twiga Stars mara mbili, mara moja Ethiopia timu ikifuzu AFCON kwa kuwafunga WAHABESH kwao Addis Ababa wakati huo wakiwa timu bora na Cynthia alikuwa mmoja wa wachezaji walifanya kazi kubwa.

Afrika Kusini pia, aling'ara kiasi cha timu kadhaa kumuulizia. Ninaamini leo Yanga anacheza na wadogo zake sana lakini bado anang'ara. Maana yake anatunza kiwango CHAKE. Na anapaswa KUPONGEZWA kwa kulinda kiwango chake zaidi.
SABABU YA KUMPA VIATU

Lengo la kumpa viatu huyu binti ni Imani ya kibinadamu kutokana na dhihaka na shambulio la kimuonekano, lakini kukumbusha uzalendo au KUFUNDISHA kuhusiana na Utaifa... MOJA
Waliomdhihaki waliangalia zaidi kuhusiana na ushabiki wa Yanga na Simba lakini unaojumuisha wote hawa ni Utaifa, yaani UTANZANIA... hatuwezi kuwanyenyekea wachezaji wa Nchi nyingine huku tukiwabeza wetu... PILI...
Huyu binti ni kati ya wachezaji waliopambana leo soka la Wanawake liko hapa, ameiwakilisha Tanzania AFCON, kwa kifupi ameipigania nchi tena wakati huo hata Ligi ya Wanawake haikuwepo, hatuwezi KUMDHARAU.

TATU
Kwa nini tuna attack personality za watu, muonekano wa mtu ni majaaliwa ya Mungu, vipi tumseme vibaya kwa muonekano wake.

Nani kati yetu amejiumba, Nani anajiona yeye ni mzuri kuliko wote? TUSIIKOSOE KAZI YA MUNGU.

MAONI YANGU
Kama ni ushabiki basi uwe kwa ajili ya klabu na si Watu au muonekano wao kwa kuwa huo hauchezi na wala hauhusiani na mpira. Tusiwatishe Dada zetu wengine kuingia kwenye soka wakati wana VIPAJI kisa watachekwa... Vizuri TUKASHABIKIA MPIRA NA HAIBA ZA WATU.... NAWATAKIA WAPENDA MICHEZO WOTE HERI YA SIKUKUU YA KRISMAS..

Na Saleh Ally

3 COMMENTS:

  1. Ukitoa msaada usiutangaze.Kujitangaza ni kumdhalilisha anayesaidiwa.Kumpa viatu nä kujitapa ni kuzidi kumdhalilisha huyo mchezaji na kutafuta kiki.Angekuwa na nia nzuri huyo aliyetoa angebaki kimya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Japokuwa huwa simfagilii Saleh kutokana na aina ya uandishi wa habari zake katika hii blog lakini katika hili nitakuwa upande wake kwa sababu amebidi atoe ufafanuzi na kumpa moyo huyo mchezaji kutokana na dhihaka alizofanyiwa kipindi kifupi kilichopita kufuatia viatu alivyovaa.Alichofanya ni kuwakumbusha hao waliomdhihaki kuwa walipaswa kumpa msaada kutokana na mapungufu waliyoyaona na sio kumdhihaki.

      Delete
  2. Hongera sana kaka salehe kwa kujali na kuthamini utu na ubidadamu wa mtu......mungu akuzidishie.......hao wanaomdhihaki mbona kuna wengine nao wana mapungufu yao kama ualbino na kadhalika lakini bado watu wanawajali na kuwaheshimu pasipo kujali kasoro zao,lakini wao wanaziona za wenzao.....leo nimepata maana halisi ya ule msemo"NYANI HAONI KUNDULE".Endelea hivyohivyo kaka kuwaelimisha kwa vitendo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic