MBWANA Samatta nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambaye anakipiga kwenye timu ya Genk huko nchini Ubelgiji jina lake limetajwa kwa wale wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kitu cha kujivunia na kinapaswa kiwape hasira wachezaji wetu wengine.
Tunamuona Samatta namna anavybadilika na kukubali kujifunza kila saa kila wakati akiwa na timu yake ya Genk na hata akiwa na timu ya taifa kitu ambacho wachezaji wetu wengi wa ndani wanakikosa kwa kujisahau na kufikiri kwamba kucheza timu ambazo wanazipenda kutawapa mafanikio ya jumla hapana kuna mambo yamebadilika.
Samatta ni mchezaji wa kawaida kwa level zetu lakini ule ukawaida wake ameweza kuutumia kwa umakini jambo ambalo wengi wanashindwa kufanya hasa kwa wakati huu ambao teknolojia inazidi kukua na soka likizidi kutazamwa na wengi wanashindwa kufanya.
Kutajwa kwake na kushindanishwa na wachezaji wenye majina makubwa ikiwa ni pamoja na Mohamed Salah, Sadio Mane wote wanaokipiga ndani ya Liverpool kwenye Ligi Kuu ya England sio hatua ya kubeza.
Mchezaji Mane leo anakula sahani moja na Samatta ni kitu kikubwa na kinachofikirisha kwamba kutoa wachezaji wengi nje kuna manufaa na matunda yake ni haya ambayyo tunaanza kuyaona.
Samatta amefungua njia wachezaji wengine mna jambo la kujifunza kutoka kwake ili kuongeza idadi ya ushindani ndani ya kuwania tuzo kubwa zikitokea tena wakati mwingine.
Tunaona kwamba Liverpool wao wametoa wachezaji wawili ambao ni Mane na Salah basi ifike wakati wachezaji ambao watachaguliwa wanaokipiga nje iwe wachezaji watatu kutoka Tanzania.
Inawezekana endepo wachezaji wetu wataamua kujituma na kufanya kazi kwa juhudi bila kuangalia nani anasema nini ama wakacheze timu gani hakuna anayefanikiwa kwa kuchagua aina ya maisha.
Kwa hili ambalo limemtokea Samatta hata akishindwa kubeba tuzo sio mbaya japo ni maombi yetu atwae kabisa na hiyo tuzo aipeleke Mbagala ambako ndipo maskani yake ilipo.
Ikitokea ameshindwa ni suala la kukubalina na matokeo kisha kujipanga upya kwa wakati mwingine kwani kushindwa ni sehemu ya matokeo kwenye soka.
Pia tumeona kwa wchezaji wa ndani ambao wanawania tuzo hiyo yumo Meddie Kagere anayekipiga Simba ambaye ni raia wa Rwanda na Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa anakipiga Ittihad yeye ni raia wa Uganda.
Okwi aliwahi kucheza ndani ya Simba msimu uliopita kwa sasa ameondoka ndani ya Simba anaendelea na maisha yake nje ya Simba lakini anafuatiliwa na ametajwa kwenye tuzo hii.
Hapa kuna kitu cha kujifunza kwa timu zetu namna zinavyofanya usajili kwa kuangalia aina gani za wachezaji wanapaswa waendelee kuwepo ndani ya timu ama kuachana nao.
Haina maana kwamba nawasema mabosi wao kwamba walikosea kumuacha hapana kuna wakati ni lazima ukubali kwamba hata kama mchezaji anahitaji dau kubwa kiasi gani na ni muhimu haina namna ni lazima uvunje tu benki.
Yote kwa yote kutajwa kwa hawa wote wa kigeni kuna jambo la kujiuliza kwa wachezaji wetu wa Bongo kwani wao wanacheza ligi ya wapi?
Muda wao wa kupambana ili wakati ujao wawe miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo kwa wachezaji wa ndani na sio kujivunia eti mchezaji aliwahi kucheza Simba ama Yanga sio sawa.
Ikumbukwe kuwa wakati timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inafungwa na Libya lawama nyingi zilielekezwa kwa Samatta kutoka kwa mashabiki.
Wapo sahihi kwa kile ambacho wanakisema kwa kuwa wanamfuatilia na kumpenda mchezaji wao hivyo wanaona kuna kitu ambacho kinakosekana kwakwe akiwa na timu ya taifa.
Kwa kuwa maoni ya wadau yalimfikia Samattta mwenyewe alikiri kulipokea na kukubali kuyafanyia kazi maoni aliyoyayapokea na aliweka wazi kwamba wadau hawajaridhishwa na kile alichokifanya.
Kwa lugha ya mtaani tunasema alikubali kupokea ujumbe kwamba alizingua kwenye timu ya taifa hakukasirika aliweka wazi kwamba ameyapokea maoni na atayafanyia kazi.
Inaonyesha namna gani yupo tofauti na wengine, nakumbuka kuna mchezaji mmoja aliwahi kuambiwa kwamba amechuja akawa mkali.
Lugha yake aliyotumia kuwajibu mashabiki haikuwa ya kiungwana alidai kwamba anaonewa kumbe alisahau kwamba mpira ni mchezo wa wazi na mwisho wa siku tulishuhudia anguko lake.
Kinachotakiwa kufanyika kwa wachezaji wetu wa Bongo ni kujifunza na kufuata kile ambacho wanashauriwa kwani anayekushauri leo kwamba umefeli ina maana kwamba anakufuatilia kwa muda mrefu.
Hawezi kukurupuka kutoka kusikojulikana na kudai kwamba umezingua ilihali hakujui wachache sana huwa wanafanya hivi lakini bado kuna umuhimu wa kuchukua maoni yao na kuyafanyia kazi.
Kwa yule ambaye hapendi kukosolewa ni rahisi kwake kupata anguko kwani ataamini kwamba yeye anajua kila kitu jambo ambalo halina ukweli katika maisha.
Maisha ya soka yana kupanda na kushuka katika haya yote mashabiki ni washauri wao jambo ambalo litawafanya wazidi kuwa bora katika kile ambacho wanakifanya siku zote bila kukoma.
Endapo Samatta angepuuza yale ambayo mashabiki wake wanamwambia huenda angeshindwa kujua wanahitaji nini na kitu gani ambacho anakosea kwa sasa hasa kwa mashabiki.
Ukweli ni kwamba kuna wakati mpira humkataa mchezaji kutokana na siku kuwa tofauti ila kinachotakiwa kwa mchezaji ni kupambana kwa ajili ya mafanikio yake na timu kiujumla.
Tunaona kwamba Stars imeshindwa kupata matokeo mbele ya Libya hii isiwaumize jumla mashabiki na kuamua kujiweka pembeni bado safari ipo na kazi inaendelea.
Wahenga walisema kuwa kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi kwa hatua ya kwanza kazi haijaisha bado inaendelea na mechi zipo mkononi mwa Stars kufuzu ni suala la muda tu.
Soka lina njia zake na ushindani upo kwani Afcon kila taifa linapenda kufika hata Tanzania pia inapenda kushiriki tena ili kuongeza uzoefu ukizingatia kwamba ilianza kuonja utamu wa kushiriki.
0 COMMENTS:
Post a Comment