December 22, 2019

KIUNGO wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa kikubwa kilichowapa matokeo chanya ni ushirikiano na kujituma kwa wachezaji mwanzo mwisho.

Simba leo imeshinda mabao 6-0 dhidi ya Arsusha FC kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho hatua ya 62 uliochezwa uwanja wa Uhuru.

"Tulikuwa 'seriaz' na mechi leo uwanjani wa na kila mmoja alikuwa anatambua kazi yake ya kufanya na shukrani kwa benchi la ufundi kwa hiki ambacho wametufundisha," amesema.

Kwa upande wa Arsuha United, Ajib Mohamed mshambuliaji wa amesema kuwa kilichowashinda kupata matokeo mbele ya Simba ni ukubwa wa timu ya Simba pamoja na makosa waliyoyafanya ndani ya uwanja.

"Tumeshindwa kupata matokeo kutokana na ukubwa wa timu ya Simba pamoja na makosa tuliyoyafanya ndani ya uwanja," amesema.

Mabao ya Simba yalifungwa na Clatosu Chama,dk 18,Gerson Fraga dk 24 akimalizia asisiti ya Ibrahim Ajibu, dk ya 33 Deo Kanda asissti ya Ajibu, Ajibu dk ya 33 asisiti Chama, Medie Kagere dk ya 57 na Francis Kahata asisiti ya Kanda dakika ya 66.

6 COMMENTS:

  1. Aibu za mzee wa Uchebe yaani Ausems kocha wa zamani wa Simba zinaanza kufichuka. Hawezekani vitimu kama hivi vinacheza na Simba halafu Simba inapata ushindi wa kuchechemea au hata kufungwa.

    ReplyDelete
  2. Welldone Mnyama.This is Simba next level

    ReplyDelete
  3. Simba sio kama Yanga ambayo Bila ya wachezaji wapya wataosajiliwa na nyota kadha mfano wa Akina Bocco, Ndemla, Mzamiru, Manulna na wengineo, wamewachapa Arusha 6 ziro

    ReplyDelete
  4. Endelea kuchonga,mtashangaa hivyo hivyo

    ReplyDelete
  5. Yanga ya sasa in genge la wahuni. Kuanzia matajiri,viongozi, benchi,wachezaji hadi mashabiki wanaandaa timu kwa ajili ya Simba tu. Halafu wakipoteza sijui watasemaje

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic