December 27, 2019


OLE Gunnar Solsjkaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa mchezaji wake Mason Greenwood uwezo wake unafanana na nyota wa zamani wa kikosi hicho anayekipiga Juventus, Cristiano Ronaldo.
Solsjkaer ameyasema hayo baada ya nyota huyo mwenye miaka 18 kufunga moja ya bao kwenye mchezo wa Ligi Kuu England mbele ya Newcastel United dakika ya 36 wakiwa ugenini kwenye ushindi wa mabao 4-1.

Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Anthony Martial aliyefunga mawili dakika ya 24 na 51 pamoja na Marcus Rasford dakika ya 41 huku lile la Newcastel United likifungwa na Matty Longstaff dakika ya 17
"Ana vitu vingi mguuni mwake na uwezo wake unalingana na Ronaldo endapo atajituma zaidi atakuwa bora zaidi ya hapa kwa sasa.
"Ronaldo alikuwa anafunga kwa miguu yake yote miwili na hata mabao ya kichwa anafunga pia ndivyo ambavyo anavyo Greenwood.
"Simpi asiliamia 50-50 labda 60-60 kutokana na uwezo wake uliopo kwenye miguu yake, ni mwepesi kutengeneza hatari na kumalizia kwa miguu yake yote miwili," amesema,. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic