December 27, 2019


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa kilichoipa ushindi mbele ya Azam FC  ni kujituma kwa wachezaji wake mwanzo mwisho ndani ya uwanja bila kuchoka.

Azam FC ilipoteza mchezo huo ikiwa ugenini kwa kufungwa bao 1-0 na Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Tanga lililopachikwa na Haji Ugando dakika ya 54 baada ya mabeki wa Azam FC kujichanganya wenyewe kuokoa pasi ya nahodha Bakari Mwamnyeto wa Cosatal Union.

"Ilikuwa ni mechi ngumu na kila mmoja alijua kwamba mambo yatakuwa magumu, wachezaji walipambana mwanzo mwisho na hakuna ambaye alikata tamaa hivyo pongezi nazirudisha kwa wachezaji," amesema.

Ushindi huo unaifanya Coastal Union kufikisha jumla ya pointi 20 ikiwa nafasi ya tano na Azam FC inabakiwa na pointi 20 ikiwa nafasi ya tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic