December 30, 2019


FT: Yanga 1-0 Biashara United
Uwanja wa Taifa

Zinaongezwa dakika tatu
Dakika ya 84 Yanga inaandika Goooool la kuongoza kupitia kwa Tariq Seif anayemalizia pasi ya Papy Tshishimbi

Dakika ya 73 Mlinda mlango wa Biashara United anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 70 Ngasa anatoka anaingia Papy Tshishimbi
Dakika ya 63 Biashara wanapiga kona haileti matunda

Dakika ya 53 Biashara wanaotea
Dakika ya 50 mlinda mlango wa Biashara United anapewa huduma ya kwanza baada ya kugongana na mchezaji wa Yanga.

Dakika ya 48 Biashara United walifanya jaribio halikuzaa matunda.
Kipindi cha pili kimeanza kwa sasa Uwanja wa Taifa.

Zinaongezwa dakika 2

Dakika ya 43 Adeyun anafanya jaribio ambalo halizai matunda.

Dakika ya 41 Biashara United walipata faulo haikuzaa matunda.

Dakika ya 33 David Molinga anapaisha faulo baada ya Feisal Salum kuchezewa rafu dakika ya 32. 

Dakika ya 20 Mrisho Ngassa ambaye amevaa kitambaa cha unahodha anapaisha mpira juu akiwa ndani ya 18.
Mechiya Ligi Kuu Uwanja wa Taifa, leo Desemba, 30 ni kati ya Yanga dhidi ya Biashara United.

Kwa sasa ni kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mpinzani.

Mashabiki wamejitokeza kiasi chake kushuhudia burudani kutoka kwa timu hizi mbili uwanja wa Taifa.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic