December 31, 2019



CHARLSE Mkwasa, Kaimu Kocha wa Yanga amesema kuwa haikuwa rahisi kupata ushindi mbele ya Biashara United kwani vijana walipambana kupata matokeo chanya.

Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Biashara United kwenye mchezo uliochezwa jana, Desemba 30 uwanja wa Taifa lililofungwa na Tariq Seif.

"Tulikutana na upinzani mkubwa kwani kila timu inapocheza na Yanga huwa inapambana mwanzo mwisho jambo linaloongeza ugumu kwetu kushinda.

"Nawapongeza wachezaji na mashabiki ni mwendelezo mzuri na tutaendelea kupambana kupata matokeo chanya," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic