MWENYEKITI wa Yanga, Dk Mshindo Msolla, ameweka bayana kuwa, kwa kutambua ukubwa wa mechi yao dhidi ya Simba, wamejipanga kuweka maandalizi maalum kwa ajili ya mechi hiyo kuona wanapata matokeo mazuri katika mpambano huo.
Msolla ameweka wazi hayo, zikiwa zimebakia siku tano kabla ya uongozi wake kuwakabili wapinzani wao Simba kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya ligi ambayo itapigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Msolla amesema kwamba wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo na kwa upande wao wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo huku wakipambana kufanya vizuri.
“Tunajua hii ni mechi kubwa sana kwa pande zote mbili na katika mechi zote 38 ambazo timu inacheza lakini mechi hizi mbili kati ya timu hizi ni muhimu zaidi kwa kila upande.
“Kwetu tunaendelea na maandalizi na tuko tayari kwa ajili ya mechi hii. Tunajiandaa kipekee kwa kuona tunaendelea kupata matokeo mazuri ambayo tumekuwa nayo katika mechi nyingine zote,” alisema Msolla.
Haihitaji maandalizi yoyote kwa ile kocha Mkwasa keshasema Simba ni timu ya kawaida. Ingieni muondoke na point 3 kwa urahisi wapewe wachezaji magodoro mliowaahidi
ReplyDeleteMikia tufc mtafungwa
DeleteWeka mke kama kawaida yenu.
ReplyDelete