December 23, 2019


BONIFACE Mkwasa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hana hofu na mchezo wake dhidi ya Simba kwani ni timu inayofungika bila wasiwasi.

Mkwasa aliongoza kikosi chake kushinda mabao 4-0 mbele ya Iringa United kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho kesho ana kibarua mbele ya Mbeya City mchezo wa ligi utakaochezwa uwanja wa Sokoine.

"Kwa sasa bado mechi yetu dhidi ya Simba ipo mbali kwani tuna mechi nyingi za kucheza kwa sasa ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Mbeya City, hivyo tusubiri na tuone itakuaje ila sina hofu na mchezo huo wa Januari 4, 2020 kwani Simba inafungika." amesema.

Yanga msimu uliopita mbele ya Simba iliambulia pointi moja baada ya kutoka sare kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa taifa na ile ya pili ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.

3 COMMENTS:

  1. Mbona muna haha kusajili wachezaji kwa ajili ya mechi na Simba??

    ReplyDelete
  2. Kumbukeni tarehe 04/01/2020 mnakutana na Mnyama siyo Iringa United

    ReplyDelete
  3. Tutaiona hiyo yanga mpya trh4/1/2020

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic