December 24, 2019




JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wote wa Yanga kwa sasa ni kitu kimoja jambo linalowapa nguvu ya kushinda mechi zao zote zilizo mbele yao ikiwa ni pamoja na ile ya watani wa jadi itakayopigwa Januari 4, Uwanja wa Taifa.

Yanga kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha msaidizi Boniface Mkwasa ambaye amekiongoza kikosi hicho kupenya hatua ya 62 ya michuano ya Shirikisho kwa kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Iringa United.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa wachezaji wamekuwa na morali kubwa kutokana na sapoti ambayo wanaipata kutoka kwa mashabiki jambo ambalo linawafanya wazidi kupambana kupata matokeo chanya.
“Kazi yetu ni kubwa na ngumu kutokana na ushindani ambao tunaupitia kwa sasa, tuna mechi nyingi ngumu na zote ni muhimu kwetu kushinda hilo ndilo tulilokubaliana hata mechi yetu dhidi ya Simba tunahitaji pointi tatu.
“Ushindani uliopo kwenye ligi tunautambua na kila mchezaji hilo ameliona jambo ambalo linatufanya tuzidi kupambana muda wote kupata ushindi, mashabiki watupe sapoti,” amesema Abdul. 

Yanga leo itashuka uwanjani wa Sokoine kumenyana na Mbeya City mchezo wao wa tisa wa ligi kuu ikiwa ipo nafasi ya 9 na pointi zake 17 inamenyana na Mbeya City iliyo nafasi ya 10 na pointi zake 8.

1 COMMENTS:

  1. Mbeya city ni vibonde vya Yanga hapo Yanga watapeta tu ila Yanga waendelee tu kujipa moyo kwa Simba timu ambayo wachezaji wake wengi wamekaa pamoja kwa muda mrefu.Ukiangalia hata wale Brazil wapo tofauti kabisa wanaonekana kuyazoea mazingira ya Tanzania. Gadiel Michel,Mohammed Hussein, shomari kapombe,muzamili Yasin,Mkude baadhi tu ya wachezaji ambao panga pangua wakiamshwa usinguzini kucheza na Yanga basi wanajua nini ya maana ya mechi hiyo. Yanga katika mechi hiyo wategemee maajabu tu lakini kazi wanao kuondoka na point.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic