December 27, 2019


BONIFACE Mkwasa ,Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa anaona fahari kutibua rekodi ya Tanzania Prisons ndani ya Ligi Kuu Bara ya kucheza mechi 12 bila kupoteza.

Prisons iliyo chini ya Adolf Richard ilicheza jumla ya mechi 12 bila kupoteza ambapo ilishinda nne na ililazimisha sare nane leo imepoteza kwa mara ya kwanza mchezo wake wa 13 kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa Samora.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga lilipachikwa dakika ya tano na Patrick Sibomana baada ya mabeki wa Prisons kujichanganya kuokoa hatari iliyoanzishwa na Abdulaziz Makame ambaye alirusha mpira mrefu uliozama ndani ya 18.

Mkwasa amesema:"Nilitambua aina ya timu ambayo ninacheza nayo namna ilivyo na falsafa zake hivyo ninaona fahari kutibua rekodi yao nzuri ambayo waliiweka kwa muda mrefu, tulikuwa tunahitaji pointi tatu hakuna jambo lingine," amesema.

Kwenye mchezo wa leo ulitawala ubabe mwanzo mwisho ambapo ilipelekea mchezaji wa Prisons Idd Buma kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa jumla ya kadi mbili za njano kutokana na kucheza rafu.

4 COMMENTS:

  1. Tawi la Mikia limekatwa leo,panga Mona chali!!

    ReplyDelete
  2. Alietoa wazo la kumfukuza kazi Ausems kaikoa Simba.

    ReplyDelete
  3. NA ALIETOA WAZO KWAMBA ZAHERA AFUKUZWE PIA AMEIPONYA YANGA KUSHUKA DARAJA KWA AIBU KUBWA.PUMBAVU ZAKO UNALETA MCHEZO HAPA UKINYA SISI TUNAHARISHA KABISA TENA FUNGA BAKULI LAKO NA UJIFANYIE TATHMINI IKIWEZEKANA NENDA KWA YULE BABU YAKO AKALOGE ILI MPATE MATOKEO,ILA KWA YANGA HII ILIYODHAIFU KIASI HICHI MBONA KICHAPO KITAWAHUSU TENA MTAYAOGA WATANI,POOOOVVVVVUUUUU RUKSAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic