NYOTA wa zamani wa Yanga, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ amesema baadhi ya wachezaji walicheza chini ya kiwango na kusababisha timu hiyo kung’olewa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi katika Uwanja wa Amaan Visiwani, Zanzibar.
Mchezo huo uliochezwa juzi, Yanga walifungwa kwa penalti 4-2 baada ya mchezo huo kukamilika dakika 90 kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Malima aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa nyakati tofauti Yanga na Simba akimudu nafasi ya mlinzi wa kati alisema wachezaji walipaswa kumaliza mchezo ndani ya dakika 90, lakini kucheza kwa kuwadharau wapinzani na kutokujua thamani na ukubwa wa klabu wanayoichezea, walijikuta walishindwa kutinga fainali.
“Baadhi ya wachezaji walicheza chini ya kiwango ni moja ya sababu iliyochangia timu kungo’lewa katika hatua ya nusu fainali na Mtibwa na walikuwa na kila sababu ya kumaliza mchezo ndani ya dakika za kawaida,” alisema Malima Malima alisema inasikitisha huku akitolea mfano penalti iliyochezwa na Abdulaziz Makame ambayo alishindwa kufunga.
Malima amewataka wachezaji wa timu hiyo na timu nyingine kucheza kwa kujituma kama kazi yao ya kujiingizia kipato pia kuonesha thamani yao wakijua timu kubwa zinafuatiliwa na mamilioni ya watu na wanatumia gharama kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment