January 10, 2020

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hauna mashaka na mchezo wa leo dhidi ya Simba kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kuwa wameinyoosha mara nyingi Simba.

Azam FC leo itakuwa kibaruani kumenyana na Simba iliyopoteza ubingwa mwaka 2018 kwa kuchapwa mabao 2-1 na Azam FC kwenye mchezo wa fainali.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Mudhathir Yahya na lile la ushindi likifungwa na Obrey Chirwa huku lile la kufutia machozi kwa Simba likifungwa na Yusuf Mlipili kwa kichwa akimalizia kona ya Shiza Kichuya.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abulkalim Amin 'Popat' amesema kuwa wana uzoefu na Simba licha ya kuwa timu imara ila watapambana kupata matokeo.

"Tuko kamili kwa mapambano pia leo tutakapokutana nao kwenye nusu fainali ya michuano hiyo mechi za nyuma tulipokutana nao tuliwafunga, tuna amini itakuwa kazi ngumu ila tupo tayari," amesema.

Mshindi wa leo atakutana na Mtibwa Sugar kwenye fainali ya Januari 13 itakayochezwa Visiwani Zanzibar na bingwa mtetezi ni Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic