UONGOZI wa Polisi Tanzania umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi, kesho Januari, 11,2020 kuipa sapoti timu yao mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.
Polisi Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu Malale Hamsini ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Biashara United juzi, itakutana kesho na Kagera Sugar ikiwa nyumbani.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa ni muda wa mashabiki kuipa sapoti timu yao kwani ni muda wa kushuhudia ushindani wa kweli.
"Kiingilio kwenye mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar ni buku tatu tu (3,000) mashabiki tujitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yetu," amesema.
Polisi Tanzania ipo nafasi ya 10 ikiwa imecheza mechi 15 imejikusanyia pointi 21 kibindoni na wapinzani wao Kagera Sugar wapo nafasi ya nane wakiwa na pointi 24.
0 COMMENTS:
Post a Comment