January 14, 2020


Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame mwaka huu yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, imeelezwa.

Simba ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Yanga ilimaliza katika nafasi ya pili
msimu uliopita wana nafasi ya kushiriki mashindano hayo.

Katibu Mkuu wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholas Musonye, alisema uamuzi huo umepitishwa rasmi katika mkutano mkuu wa baraza hilo uliofanyika Desemba mwaka jana.

Musonye ambaye ataachia ngazi nafasi hiyo baadaye mwaka huu alisema mashindano ya Kombe la
Chalenji yatafanyika Sudan wakati ya wanawake yatacheza Rwanda pamoja na michuano ya kusaka
tiketi ya kushiriki fainali za vijana za wasichana za umri chini ya miaka 17 kwa ukanda huu.

Alisema mashindano ya wanawake ya umri chini ya miaka 20 yatafanyika Uganda wakati yale ya
wavulana ya umri chini ya miaka 16 yakipelekwa Djiboiti na Burundi itakuwa mwenyeji wa michuano ya wavulana ya U-20 pamoja na U-17 wasichana.

Aliongeza kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Cecafa iliyoko chini ya Rais wa baraza hilo, Wallace Karia,
iliteua Kamati ya Mashindano ya watu watano ambao watafanya kazi kwa kushirikiana na Ofisa
Mtendaji Mkuu atakayekuja ili kufanya majukumu ya kila siku.

1 COMMENTS:

  1. Ninavyojua labda Musonye ang'atuke,kama ataendelea kuwa kiongozi Yanga atawasikia bombani,ana kauli za kuudhi,hawatashiriki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic