January 1, 2020


TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, KMC, inapita kwenye kipindi kigumu ambapo haijapata ushindi kwa muda wa siku 56 kwenye mechi sita ilizocheza sawa na dakika 540 kabla ya kuingia mwaka mpya 2020.
Mara ya mwisho KMC kuambulia pointi tatu ilikuwa Novemba 4, 2019 ilipomenyana na Biashara United Uwanja wa Uhuru jijini Dar ambapo ilishinda kwa mabao 2-1 yaliyofungwa na Serge Alain na Kenny Ally. Baada ya hapo, haijaonja ladha ya ushindi zaidi ya kuambulia sare na vipigo.
Kwenye jumla ya mechi sita mfululizo ambazo KMC ilicheza baada ya kupata ushindi mbele ya Biashara United, imepoteza mechi tano na kuambulia sare moja pekee mbele ya Yanga Uwanja wa Taifa, Dar, mechi iliyochezwa Desemba 2, mwaka 2019.
Ilipoteza mbele ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 2-1, Alliance FC 2-1 KMC, Mbao 2-1 KMC, Polisi Tanzania 2-1 na KMC 0-2 Simba. Katika mechi hizo sita, imefungwa mabao 11 na kufunga mabao manne.
Matokeo hayo yanaifanya iwe nafasi ya 17 na pointi zake tisa, Jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mwadui na inasalia nafasi ya 17 ikiwa na pointi 10.
Kaimu Kocha Mkuu wa KMC, Ahmad Ally amesema kuwa matokeo hayo mabovu yanawamumiza kwani sio malengo yao.

1 COMMENTS:

  1. Hiyo ni lazima kwa sababu ukiisha ifunga au kutoka draw na yanga tuu basi hamna namna ya ushindani zile hela zimeisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic