Kiungo wa Simba mwenye uraia wa Brazil, Gerson Fraga, amesema anatamani kucheza mechi ya wapinzani wao wakubwa hapa nchini timu Yanga, huku akitamba kuipa ushindi timu yake pindi atakapocheza mechi hiyo.
Fraga alisajiliwa na Simba katika dirisha kubwa la usajili sambamba na Wabrazili wenzake, Tairone Santos na Wilker Henrique ambao wote kwa pamoja hawajawahi kucheza mechi dhidi ya Yanga.
Fraga alisema kuwa anatamani kuona anapata nafasi ya kucheza mchezo huo ambao kwake utakuwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo.
“Kila mtu huwa anatamani kushiriki katika mchezo dhidi ya mpinzani wake mkubwa katika ligi husika, mimi sijawahi kushiriki mechi hii kwa kuwa ndiyo mechi ya kwanza Simba itacheza mimi nikiwa mchezaji wake, hivyo natamani sana kuona napata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza.
“Ni mechi kubwa yenye presha kubwa, kwangu siogopi kuanza katika mchezo huo kwani ndiyo kwanza natamani kucheza ili kuhakikisha naipa ushindi timu yangu.
“Sisi kwa pamoja tunataka kuwapa raha mashabiki wetu wote kupitia ushindi mzuri tutakaoupata,” alisema kiungo huyo. Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza katika mechi ya mzunguko wa kwanza kwenye ligi kuu, ambapo mechi hiyo inatarajiwa kufanyika Januari 4, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Usihofu utacheza ila kaza msuri tu this is simba
ReplyDelete