January 2, 2020


Baada ya kufunga bao lake la kwanza katika Klabu ya Yanga, ambalo liliipa timu hiyo ushindi mbele ya Biashara United, mshambuliaji mpya Tariq Seif, amesema kuwa sasa atafunga kwenye kila mchezo atakaopata nafasi ya kucheza.

Tariq aliibuka shujaa baada ya kufunga bao dakika za mwisho lililoipa ushindi Yanga dhidi ya Biashara kwenye mchezo uliochezwa  Jumatatu ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar na kuisaidia timu hiyo kuvuna alama zote tatu na kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 24.

Tariq alisema kuwa kitendo cha kufunga bao la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Biashara United, kimempa moyo zaidi wa kufanya makubwa kwenye klabu hiyo ambapo kwa sasa atajituma zaidi ili awe anafunga kwenye kila mchezo atakaopata nafasi ya kucheza.

“Kiukweli bao ambalo nilifunga jana (juzi) limeniongezea nguvu sana ya kupambana, unajua nilikuwa nimekaa nje kwa muda mrefu bila kucheza, kwa hiyo kitendo cha kurudi uwanjani na kufunga kimenipa moyo na sasa nitaongeza juhudi zaidi ili niweze kufunga kwenye kila mchezo,” alisema Tariq.

Kauli ya Tariq inakuwa kama inaibua hofu Simba kutokana na kuwa atakuwa anakutana dhidi yao Januari 4, mechi itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tariq amejiunga na Yanga wakati huu wa dirisha dogo la usajili akitokea katika Klabu ya Dekernes inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri, lakini pia alishawahi kupita katika klabu ya Stand United na Biashara United zote kutoka Tanzania. 

2 COMMENTS:

  1. Tuseme siku hiyo Ingekuwa si uwepo wa Tariq Yanga ilikuwa iondoke na point moja tu kibindoni kwa goli la lala salama

    ReplyDelete
  2. jamani acheni mpira wa maneno alisha cheza na simba sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic