PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa mpango mkubwa wa kikosi hicho ni kuboresha kikosi chake ili atetete ubingwa wa Ligi Kuu England.
Guardiola amesema kuwa hatazami ameachwa kwa jumla ya pointi ngapi isipokuwa anatazama ni namna gani atapata matokeo kwenye mechi zake anazocheza ndani ya uwanja.
"Sifikirii kuhusu kuachwa na mpinzani wangu ama kuwa na pointi ngapi kwa sasa ila kikubwa ni kuona ni namna gani nitapata matokeo chanya ndani ya uwanja yatakayonisaidia kutetea ubingwa," amesema.
Leroy Sane mchezaji wa City ana nafasi kubwa ya kuondoka ndani ya kikosi hicho msimu huu kwenye dirisha la usajili ambalo limefunguliwa leo.
City imecheza mechi 20 ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 41 imeachwa kwa jumla ya pointi 14 na Liverpool walio nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 55 na wanamchezo mmoja mkononi kwa kuwa wamecheza mechi 19 ndani ya Ligi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment