UONGOZI wa Singida United umefunga mwaka 2019 ukiwa haumani
unachokiona baada ya kuvuna pointi saba kwenye jumla ya mechi 13 ambazo ni sawa
na dakika1170.
Ramadhan Nswanzurimo ndiye Kocha Mkuu wa kikosi hicho, leo
ataiongoza timu yake mbele ya Azam FC, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,alitwaa
mikoba hiyo kutoka kwa Felix Minziro ambaye hakuongezwa mkataba wake baada ya
kuibakiza kwenye ligi msimu wa 2018/19 na sasa yupo na timu ya Pamba FC
inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Kwenye mechi 13 ambazo zina jumla ya pointi 39, Singida United
imepoteza jumla ya pointi 32 ikiwa imeshinda mechi moja tu mbele ya Mbeya City
na imepoteza mechi nane na kulazimisha sare nne pekee ndani ya mwaka 2019 na
haijapata ushindi kwa miezi miwili mfululizo, Septemba na Oktoba na ule wa mwezi
Novemba ambao ilishinda mbele ya Mbeya iliweka rekodi ya kuchapwa mabao 5-1 na
Lipuli ya Iringa.
Matokeo yao yalikuwa
namna hii:-Ndanda 1-1 Singida United, Septemba 9/19, Singida United 0-0 Mbao,
Septemba 25/19, Singida United 0-1 Alliance, Septemba 28, Polisi Tanzania 2-1 Singida
United, Oktoba 20,19.
Coastal Union 0-0
Singida United, Oktoba 23, Singida United 0-1 Simba, Oktoba 27, Singida United
1-2 JKT Tanzania, Oktoba 30, Mtibwa Sugar 0-0 Singida United,Novemba 2,Lipuli 5-1
Singida United, Novemba 7.
Mbeya City 0-1 Singida United, Novemba 23,Tanzania Prisons 1-0 Singida United, Novemba 25.
Nswanzurimo amesema kuwa matokeo mabovu ya kikosi hicho yanatokana na kukosa wachezaji wenye uwezo wa kutumia nafasi wanazotengeneza jambo analolifanyia kazi kwa ukaribu.
Nswanzurimo amesema kuwa matokeo mabovu ya kikosi hicho yanatokana na kukosa wachezaji wenye uwezo wa kutumia nafasi wanazotengeneza jambo analolifanyia kazi kwa ukaribu.
0 COMMENTS:
Post a Comment