Mvutano wa maneno unaendelea kati ya Afisa Habari wa Simba, Haji Manara na Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz huku kila mmoja akijaribu kuisimamisha timu yake.
Hali hiyo imekuwa ikionekana katika mitandao ya kijamii na hata katika mahojiano yao mbalimbali na vyombo vya habari, na kuleta mijadala mbalimbali miongoni mwa mashabiki wa timu hizo.
Hivi karibuni baada ya kumalizika kwa mchezo wa Yanga na Kagera Sugar na kushuhudia Yanga ikifungwa 3-0 nyumbani, Antonio Nugaz alikaririwa akisema kuwa walishindwa wenyewe kutumia nafasi walizozitengeneza, ambapo hii leo Haji Manara ameibuka na kukosoa lugha aliyotumia katika maelezo yake.
Katika ukurasa wake wa Instagram, Manara amezungumzia kauli ya Nugaz kwa utani akisema, "rafiki yangu mimi huyo, eti ku'compose', najua alikusudia ku'convert', sitachoka kumweka sawa, mzigo wangu mwenyewe huu, halafu sasa hivi nishaanza kumfundisha kuongea kwa authority, sio hyo staili yake, huku kwenye soka ukiongea Mwamba wa Pua unaukaza kidogo, hii yaani huku sio, watu wa huku hovyo kidogo".
Tambo za maafisa hao zimeanza kuelekea kwenye mchezo wao uliopigwa wiki mbili zilizopita ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2, huku ushujaa ukionekana kwa Yanga ambao waliamka na kusawazisha mabao yote mawili ndani ya dakika 10 za kipindi cha pili cha mchezo.
Wangeshinda je?hata wewe ulieandika hii habari unawaona yanga ni mashujaa kwasababu umeridhika na sare,tunashukuru kwakua mnakiri udhaifu wenu wenyewe,kadri siku zinavyokwenda mnazid kukubali kwamba yanga hakuna kitu pale,kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi,mtu ameshajifunga inamaana benchi la ufundi halioni kwamba kijana alishatoka mchezon?mlipaswa kumtoa sonso mapema sana kabla ya hata kipindi cha kwanza kuisha,mnasababisha mpaka kocha anapewa kadi,walahi msiposhtuka mkarudi kule kwa babu mtafungwa kila mechi mama zangu,poleni sana na hongerni kwa ushindi wa sonso hao ndio akina ALLY ALLY wanaendelea kufanya yao.
ReplyDelete