January 19, 2020


Kocha Mkuu wa timu ya Simba SC, Sven Vanderbroeck amewapongeza wachezaji wake baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijinI Mwanza.

Vanderbroeck alisema timu yake ilicheza kwa kupambana sana kuweza kutengeneza nafasi mbili na kuweza kuzitumia vyema. Alisema hali ya hewa ya mvua ilisababisha timu yake ishindwe kucheza mpira wake kutokana na uwanja kutokuwa kwenye hali nzuri.

Alisema Mbao FC walicheza vyema katika nafasi ya kiungo, lakini timu yao ikabadilisha mfumo na kutumia nafasi za winga pamoja na mipira ya kona jambo lilioweza kuwasaidia na kupata ushindi.

Kimsimamo, Simba inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 38 baada ya kushika dimbani mara 15. Kwa upande wake, kocha msaidizi wa timu ya Mbao FC, Abdulmutik Haji alisema timu yake ilicheza vyema licha ya kupoteza mchezo huo.

Alisema timu yake bado ina tatizo katika kutengeneza nafasi za kufunga, hivyo aliahidi wakati wa mazoezi kurekebisha tatizo hilo ili waweze kupata ushindi katika michezo yao ijayo.

Alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka wa timu yao waendelee kuipa sapoti timu yao iweze kufanya vyema katika michezo yao ya Ligi Kuu hidi ya Namungo FC utakaochezwa Februari 3 katika Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi na Februari 6 dhidi ya Ndanda SC huko Nangwanda sijaona mkoani Mtwara.

Katika msimamo wa Ligi Kuu, Mbao FC inayodhaminiwa na Kampuni ya GF Trucks iko katika nafasi ya 14 baada ya kujikusanyia pointi 18 kutokana na
mechi 17 ilizocheza hadi sasa.

2 COMMENTS:

  1. Hofu yangu ni kuwa MASHABIKI WENYE HASIRA WA YANGA MSIANZISHE KAMPENI KUDHURU MAREFA KWANI AMANI ITAONDOKA VIWANJA VYA SOKA. OMBI BODI YA LIGI NA TFF WAAMBIENI WAAMUZI WACHEZESHE KWA HAKI KWANI LA SIVYO UMEWASIKIA MASHABIKI WA YANGA NA MIKAKATI YAO!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao hata ukichezeaha kwa haki watalalamika tu, ubovu wa timu yao wanajificha kwa waamuzi kana kwamba wanaonewa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic