Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage, amesema alisaini mkataba na TP Mazembe ambao unaiwezesha Simba kupata asilimia 20 ya pesa za mauzo ya Mbwana Samatta kila anapokwenda.
Rage ameeleza hayo kupitia Kipenga ya East Africa Radio, ambapo ameweka wazi kuwa mkataba huo upo na Simba wanatakiwa kufuatilia pesa kuanzia za kuuzwa kwenda KRC Genk na sasa kama atauzwa Aston Villa.
Miaka 10 iliyopita alikuwa anachezea Simba 2010-2011.
Kuanzia 2011-2016 akachezea TP Mazembe, ambako alishinda Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe Shirikisho pamoja na kuibuka mchezaji bora wa ndani mwaka 2016.
2016 - 2020 akachezea KRC Genk ambako amechukua ubingwa wa Belgium pamoja na Super Cup huku akishiriki UEFA Champions League na Europa League.
Misimu mitatu na nusu ya Samatta ndani ya Genk, amecheza mechi 191, amefunga magoli 76 na ametoa Assist 20.
CHANZO: EAST AFRICA TV
0 COMMENTS:
Post a Comment