BERNARD
Marrison, nyota mpya wa Yanga amesema kuwa amekuja Bongo kufanya kazi ndani ya
Yanga wenyewe watampenda.
Marrison raia
wa Ghana ambaye ni mshambuliaji, ametua leo nchini Tanzania akitokea nchini Ghana kwa ajili ya
kumalizia taratibu za awali kuitumikia timu ya Yanga.
“Nimekuja
rasmi ndani ya Yanga kufanya kazi na nina amini tutakuwa vizuri kutokana na
ubora wa kikosi pamoja na sapoti ambayo tutaipata kutoka kwa mashabiki.
“Kikubwa ni
sapoti kwani hakuna jambo jingine ambalo nimekuja kufanya zaidi ya kazi tu kwa
sasa,” amesema.
Miongoni mwa
timu ambazo amezipitia nyota huyo ni pamoja na DC Motemma Pembe, Orlando
Pirates na AS Vita.
wakina molinga hao
ReplyDeleteHaya zibeni ufa
ReplyDeleteLeteni wapya kwa wingi muchukue ubingwa haraka
ReplyDeletehaya ni maneno ya waandishi na sio wachezaji, kila mchezaji akija wwaandishi wanashindwa hadi kubadilisha maneno. wanasahau kama walivyokuwa wanasahau darasani.
ReplyDeletehawa wanadanganya mashabiki na kujikuta wanachoona ni tofauti.