January 17, 2020

DILI la nyota wa Tanzania Mbwana Samatta likijibu kujiunga na Aston Villa iliyo nafasi ya 18 kwenye msimamo na pointi zake 21 anaweza kuanza na mechi kali mbili na zote atakuwa nyumbani.

Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England ipo kwenye hesabu za mwisho kukamilisha kuipata saini ya Samatta anayekipiga klabu ya Genk.

Mechi yao iliyo kwenye ratiba ni Januari 18 ambapo watacheza na Brighton ugenini hii itakuwa ngumu kwake kuanza ila zinazofuata dhidi ya Watford ya Januari 21 na Leicester City Januari, 28 kuna namna kijana anaweza kuanza endapo mambo yatakuwa sawa.

Kila la kheri Samatta, dili litimie ili bendera ya Tanzania izidi kupeperuka.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic