January 18, 2020


Imefahamika kuwa, kiwango cha mishahara ya wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi la Simba ni Sh Mil 350 ambapo kwa mwaka inakadiriwa kufi kia Sh Bil 4.

Hilo limebainika siku chache baada ya mwekezaji wa klabu hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ kusema kwa mwaka Simba inalipa wachezaji mishahara kufi kia Sh Bil 4.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mishahara hiyo ni kwa wachezaji 28 na viongozi wa benchi lote la ufundi.

Mtoa taarifa huyo alisema kiasi hicho cha fedha kimewazidi watani wao Yanga ambao wenyewe mishahara yao kila mwezi inagharimu Sh Mil 120 pekee ikijumuisha wachezaji 28.

“Maswali mengi yaliibuka mara baada ya Mo kutangaza kiwango cha mishahara anayolipa kufi kia Sh Bil 4, mashabiki wa Simba wana haki ya kuhoji katika hilo. “Ukweli ni kwamba mishahara ya kila mwezi inagharimu Sh Mil 350,” alisema mtoa taarifa huyo.

10 COMMENTS:

  1. Ml 350 kila mwezi mishahara tu bado Huduma za time na gharama za uendeshaji lakini timu inatolewa raund ya awali na UD songo inapigwa na mwadui na mtibwa. Timu inaingiza tu hasara hakuna faida yoyote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mpira Ni zaidi ya Mshahara unaosema. Barcelona au Madrid Wana kila kitu lkn wanafungwa na akina Granada ambao mishahara ya wachezaji ni karibia mara tano ya Madrid au Barca. Kwa hiyo lazima ujue kuwa ukiwekeza hata kwa pesa nyingi haimaanishi hautafungwa na timu ndogo, watu wanakutime mapema then wanapack basi utafurukuta hadi dk 90 na hujapata goli. Mshahara wanaolipwa liver Ni tofauti na Manchester lkn timu hizi Ni mbingu na ardhi.

      Delete
  2. Kayuni_E. Sidhan kama upo sawa?majibu utayapata kama utafuatilia historia ya tp mazembe,mpira haupo hivyo unvyoamin wewe,kama mungu hulaumiwa kwakuchukua viumbe wengine wakiwa na umri mdogo au kuwacheleweshea mahitaji japo wana juhudi zakiutafutaji sembuse kwa timu inayoundwa na wanadamu?yesu alipata mgogoro nafsi akiwa msalabani na ikafika mpaka akaongea"BABA IKIWEZEKANA KIKOMBE HIKI KINIEPUKE"it means alimlaumu mungu,hivyo kuna wakat ili mafanikio yaje lazima lawama ziwepo japo wengine hulaumu kwa dhamira yakukejeli,cha msingi viongozi wasiposimama imara watayumbishwa na midomo ya watu pamoja na media kama za akina saleh jembe,mwandishi anakwambia "imeripotiwa"ukiuliza chanzo hakuna sasa huoni kama ni uchochezi wa waziwazi.

    ReplyDelete
  3. Simba ilifika ilipofika na kupata sifa kimataifa ambazo zinataja ni kuwa Simba ni miongoni mwa timu bora Africa, jambo ambalo litabakia Katika historia, Jee nyie mlifika waki au kuwa matokeo yenu na Kagera yamekufanyeni mropokwe ovyo Bila kujitazama kwanza nyie wenyewe mlivo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huu usanii wa Saleh uachwe kabisa. makala za ujanja ujnja tu, alichofanya ni kugawa bilioni 4 kwa miezi 12 na kutuletea taarifa hiyo. na limutu limoja humu linalaumu eti simba imetolewa caf, hivi hadi Liverpool inabeba ubingwa ulaya timu ngapi za maana zilitolewa?

      Delete
  4. Yaani amechukua bil 4 gawanya kwa 3 tu

    ReplyDelete
  5. Hakika nijambo jema kutambua msaada wako kwa watanzania,,,mungu akubariki sana kiongoz wetu mo dewij🙏🙏🙏

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic