January 18, 2020


KOCHA wa zamani wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa amesikia kelele za mashabiki wa timu hiyo wakishinikiza uongozi umrudishe kufundisha timu hiyo lakini kwa upande wake hafikirii kurejea nchini Tanzania kwa kuwa ni wakati wa kuvuna walichopanda awali.

Aussems raia wa Ubelgiji ambaye alitimuliwa mwanzo mwa msimu huu kufuatia kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuipa ubingwa timu hiyo na kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Kocha huyo ameanza kutajwa na mashabiki wa timu hiyo wakiutaka uongozi kumrejesha kwenye timu hiyo baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa, ambapo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo alitangaza kujiuzulu kabla ya kutangaza kurejea tena.

Aussems alisema kuwa kwa upande wake haoni jambo la kushangaza kwa yanayoendelea kwenye timu hiyo kwa kuwa wanavuna walichokipanda nyuma na wala hakifirii kukubali kurejea kutokana na alichofanyiwa awali.

“Siyo jambo zuri kutaka kujua nini wanachokutana nacho Simba kwa sababu kwangu sioni kama kuna kitu kipya ambacho naweza kusema kwa kuwa wanavuna walichopanda wakati naondoka.

“Unajua katika maisha unapata kile ambacho unastahili kupata na siyo unachotaka kupata sasa na wao wamepata wanachostahili, kifupi siwezi kurejea Simba kwa sababu ilishapita naangalia mambo yangu mengi maana ni ngumu kufanya kazi na watu wasiotaka kukubali,” alisema Aussems.

4 COMMENTS:

  1. Hana lolote nani anaetaka kumprejesha Simba? Wanaompigia debe ni vilaza kama yeye. Namba hazidanganyi kocha mpya wa Simba ameshinda mechi zake tatu za kwanza zote vizuri tu wakati kocha wa Yanga aliemwagiwa misifa na usajili wa kutisha wa dirisha dogo,kutia mguu tu kachapwa tatu mtungi nyumbani. Mashabiki wa Simba ni vilaza wasiojitambua kwani wanakubali kuaminihswa na baadhi ya vilaza kuwa timu yao mbovu wakati sio kweli. Si Azam si Yanga Simba ni timu bora by far ila mashabiki wake wanaanza kupotea njia.Kwa kiasi fulani unaweza kusema kwa sasa Simba ina timu nzuri ila mashabiki wake tia maji. Wanakubali kuaminihswa na mashabiki wa Yanga kuwa wana timu mhovu kisa ushindi wa sare walioupata Yanga kwa Simba kama si ujinga kitu gani?

    ReplyDelete
  2. SALEH JEMBE ACHA UONHO BROTHER,MBONA WEWE NI MUONGO SANA KWANIN NDUGU?KELELE ZA SHABIKI ZNA MSAADA GANI KWA CLUB?KAMA ZINGEKUA ZINA MSAADA BASI SIMBA ANGESHASAJILI AKINA ELIA MESHACK NA AKINA WALTER BWALYA,ACHAGA UJINGA BROTHER,HAKUNA ANAEMTAKA UCHEBE KWASASA USITENGENEZE PSYCHOLOGICAL DEMAND ILI KUHARIBU AKILI ZA MASHABIKI KWAKUWAAMINISHA KWAMBA SIMBA NI TIMU MBOVU AU KOCHA NI MBOVU HAPANA UNAKOSEA BROTHER,AMESHASIMAMIA MECHI TATU ZA LIGI KUU NA AMESHINDA MBILI NA KUPATA SULUHU MOJA,NA NYIE HUYO WA KWENU VIP?AMESHINDA NGAPI TANGU APEWE TIMU?HII BLOG KILA KUKICHA INAZID KUPOTEZA UBORA WAKE.POLENI SANA AKINA SALEH JEMBE.

    ReplyDelete
  3. Nani kamwambia huyo Kuna mashabiki wanamtaka na kinachovuna Simba ni wimbi la ushindi analoleta mbadili wake kitu ambacho kinamuumiza vibaya. Timu iliboronga na kufungwa na Mwadui na alishindwa kuhifadhi nidhamu ambayo sasa imerejea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic