January 12, 2020

IMEELEZWA kuwa Uongozi wa Singida United kwa sasa unahaha kuwalipa madeni wachezaji wake ili kurudisha morali iliyokuwa imepotea ndani ya timu.
Singida United ambayo imefanya usajili wa wakongwe ikiwa ni pamoja na Athuman Idd Chuji, Haruna Moshi ‘Boban’ ili kuokoa jahazi bado haijawa na matokeo mazuri imeshinda mechi mbili pekee ikiwa nafasi ya 19 na pointi zake  10.

Jana ilishinda mbele ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Namfua. 
Habari zinaeleza kuwa wachezaji wengi wa Singida United wanadai malimbikizo ya mshahara wao jambo linalowafanya wacheze wakiwa na mawazo mengi wakiwa uwanjani.
“Wachezaji wanadai malipo kwa muda mrefu sasa uwezo wao hauwezi kuwa bora ndani ya uwanja kwa kuwa wana mengi vichwani mwao, kwa sasa uongozi unahaha kumalizia madeni na umepewa siku saba ili kukamilisha hayo masuala yao,” kilieleza chanzo hicho.
 Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana ambaye alisema kuwa kuhusu suala la malipo lipo juu ya viongozi, ila kutokana na matokeo wanayoyapata wanapitia kwenye kipindi kigumu watapambana kurudi kwenye ubora wao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic