SAID Ndemla
ni miongoni mwa wachezaji wazawa ndani ya Simba ambaye amekuwa na nafasi finyu
ndani ya kikosi hicho licha ya kuwa na uwezo mkubwa kwenye miguu yake na akili
za kufikiria.
Msimu
uliopita akiwa chini ya Patrick Aussems aliweza kuonyesha makeke yake kiasi
chake na kwenye mchezo dhidi ya KMC uliochezwa uwanja wa Taifa alirudisha tabasamu lake kwa muda baada ya
kufunga bao la kwanza kwenye mchezo huo akiwa nje 18.
Ugumu wa
nafasi ndani ya Simba iliyo chini ya Sven Vanderbroek kwa sasa aliyepokea mikoba ya
Aussems unatokana na kuwa na viungo wengi waliosajiliwa ikiwa ni pamoja na
Clatous Chama, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Francis Kahata na Sharaf Shiboub.
Baada ya
dirisha dogo kufunguliwa timu nyingi zimekuwa zikimpigia hesabu ikiwa ni pamoja
na Polisi Tanzania, Singida United na KMC ambao wanahitaji huduma yake,
Huyu hapa Ndemla anaweka wazi kuhusu hesabu zake na mipango yake kwa sasa:-
“Hapa nilipo
kwa sasa si kwa bahati mbaya bali inatokana na malengo ambayo ninayo kwenye
kichwa changu na bado ninaendelea kupambana kuyafikia hayo malengo.
Mipango
inakwendaje?
“Kila siku
mpya ninayoanza ninashukuru kwa Mungu na kuitazama kuwa ni siku yangu ya
mafanikio kwa kufikiria vitu vipya vya kufanya ambavyo vitanifanya nifikie
malengo makubwa.
Singida United na Polisi zinahitaji
saini yako hili lipoje?
“Kwangu mimi
kunipata itakuwa ngumu hasa ukizingatia kwamba kwa sasa nina mkataba na timu
yangu sasa sijui wao wananitaka kwa nini ila kwa kuwa ni mchezaji basi nipo
ndani ya Simba.
Unapenda kuitumikia timu gani?
“Hakuna timu
ninayoifikiria zaidi ya Simba, naskia Singida United wanasema ninaweza kuikoa
isishuke daraja, hili si kweli sina uwezo huo wa kuinusuru timu isishuke daraja
ni timu inayocheza na si mchezaji mmoja.
Ushindani wa namba unauzungumziaje?
“Kama sehemu
hakuna ushindani huwezi kuwa bora, ila kwa kuwa nakutana na ushindani huu ni
kawaida kwa mchezaji duniani kote hili suala lipo.
“Kuhusu
suala la kuanza halipo mikononi mwangu anayepanga kikosi ni kocha mwenyewe yeye
ndiye anayejua aina ya wachezaji anaowataka waanze.
Nafasi yako ipoje?
“Bado nipo
Simba na nina mkataba na Simba hiyo ndiyo nafasi yangu.
Unajiona wapi miaka mitano mbele?
“Muda bado
upo wa kupambana, najiona mbali kwani kipaji ninacho na uwezo Mungu amenipa.
Kwa nini Simba na si kwingine?
“Ndipo
ambapo nipo na ni mabosi wangu kwa sasa ndio maana nipo hapa.
Dili lako la kwenda nje lipoje?
“Hilo kwa
sasa siwezi kulizungumzia mambo yakiwa sawa litakuwa wazi.
Utakosa nini kwa Aussems?
“Kazi ya
mchezaji ni kufanya kile anachoambiwa na kocha kuhusu kumkumbuka ana mengi
ambayo tumefanya naye ila yatabaki ndani ya moyo wangu.
Unamzungumizaje kocha mpya?
“Kiukweli
kwa mwanzo ambao tumeanza naye na namna ilivyo ni ngumu kumzungumzia kocha wetu
mpya hata kumtofautisha na yule aliyepita siwezi kabisa kuzungumzia hilo lipo
juu ya uwezo wangu.
Unawaambia nini mashabiki?
“Sapoti yao
katika kila tunachokifanya ni muhimu kwani mafanikio yetu yanabebwa na
mashabiki ambao wanatupa sapoti kila mara ambapo tunakuwa.
Ushindani ndani ya ligi unakupa kitu
gani?
“Ushindani
ni mzuri kwani inaonyesha kila timu imejipanga, hata sisi tumejipanga kupata
matokeo chanya ili kufikia malengo ya timu kiujumla.
“Ubingwa ni
hesabu zetu ndio maana kila mechi kwetu ni sawa na fainali.Ligi ni ngumu kila
timu inaonyesha imejipanga ili kupata matokeo mazuri,” anamaliza Ndemla.
Safi sana Said Ndemla .Sasa nafikiri huyu kanjanja atakuacha ufanye kazi.Kila mwezi haipati Ndemla Ndemla utafikiri anakulipa mshahara au ni kocha wa Simba Ganga yako kanjanja
ReplyDeleteWelldone wa jina langu.Piga kazi achana na hao wabubujaji.Keep it up.kila la kheyr ufikie malengo yako
ReplyDelete