MASSIMILIANO Allegri, anatajwa kutazamwa kwa ukaribu na uongozi wa Manchester United ili kupewa dili la kuinoa timu hiyo endapo Ole Gunnar Solskjaer atasepa ndani ya Old Trafford mwezi ujao.
Muitalia huyo mwenye miaka 52 aliachana na Juventus msimu uliopita akiwa ameipa mataji matano ndani ya Seria A na anatafuta changamoto mpya kwa sasa.
Ripoti zinaeleza kuwa tangu kuachana na Juve, Allegri amekuwa na matumaini ya kurejea kwenye kazi yake hiyo huku akiwa na matumaini makubwa kuibukia ndani ya United.
Inaamainika kwamba, Arsenal walifanya naye mazungumzo baada ya kumpiga chini Unai Emery ili akawe kocha wao mwezi uliopita dili hilo halikutiki.
Solskjaer amekuwa hana wasiwasi wa kufukuzwa licha ya kupitia kipindi kigumu ndani ya United kwani alipoteza mbele ya wapinzani wake Manchester City kwa kufungwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Carabao na kwenye jumla ya mechi sita za mwisho ameshinda mbili pekee.
Pia aliyekuwa kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino naye anatajwa kuibukia ndani ya United ili kuokoa jahazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment