KHLEFFIN Hamdoun, kiungo mshambuliaji aliyekuwa akiitumikia Mlandege ya Zanzibar amemalizana na Azam FC kwa kusaini kandarasi ya miaka minne.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba alivutiwa na uwezo wa nyota huyo baada ya kumuona kwenye mchezo wa robo fainali wa Kombe la Mapinduzi ambapo Azam FC ilishinda kwa bao 1-0.
Huu ni usajili wa kwanza kwa Azam FC msimu huu kwenye dirisha dogo lililofunguliwa mwezi, Desemba 15, 2019.
0 COMMENTS:
Post a Comment