January 18, 2020


NICHOLAUS Wadada, beki kisiki wa Azam FC leo amepewa kazi moja ya kuigoza safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Obrey Chirwa kuimaliza Yanga ya Mbelgiji, Luc Eymael.
Wadada amekuwa ni injini ndani ya Azam FC kwa kuhusika kwenye jumla ya mabao matano kati ya 20 ambayo wamefunga Azam na ameongoza safu yake ya ulinzi kuruhusu mabao nane ya kufungwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wachezaji wote wamepewa majukumu ya kufanya ndani ya Uwanja ili kuipa timu matokeo mbele ya Yanga ikiwa ni pamoja na Wadada.
“Wachezaji wote wamepewa majukumu ya kufanya haimaanishi Wadada pekee ndiye amepewa kila mchezaji ana kazi yake ndio maana unaona timu inapata matokeo kwa kuwa wanacheza kwa kushirikiana.
“Ushindani kwenye ligi ni mkubwa nasi tunapambana kuona namna gani tutafikia malengo ambayo tumejiwekea ndani ya ligi pamoja na Shirikisho kwani kila mechi ina mtindo wake wa kipekee,” amesema Cheche.

1 COMMENTS:

  1. Nawaomba Azam asijiangushe mchezaji wa timu pinzani makusudi kwa sababu Mbeljiki huyo amesema likitokea hilo ataikimbia Yanga kwahivo afikiriwe sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic