LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Ubelgiji ana kibarua kizito cha kuzimega dakika 450 ambazo ni za moto kwake kutokana na kuanza kwake kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar.
Eymael alianza kwa kupokea kichapo cha mabao 3-0 akiwa uwanja wa Uhuru mbele ya Kagera Sugar ya Mecky Maxime, ana mechi tano ambazo ni sawa na dakika 450 leo atakuwa anazimega dakika tisini nyingine akimenyana na Azam FC , Uwanja wa Taifa mchezo wa ligi.
Januari, 22, Yanga itacheza na Singida United uwanja wa Namfua mchezo wa ligi na atarejea Bongo, Januari 24 kumenyana na Tanzania Prisons mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Uhuru.
Februari, 2 atacheza na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Uhuru mchezo wa ligi na dakika yake ya 450 ataimaliza mbele ya Lipuli Februari 5 Uwanja wa Uhuru.
Eymaela amesema kuwa atatumia muda wake kusuka upya kikosi hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa inafanya makosa mengi ya kiufundi.
Tunamrakia kla la heri injapokuwa man magum
ReplyDeletehapo atapoteza mechi 1 atasare 2 atashinda 2
ReplyDeleteAtafukuzwa huyu sio kocha bora tungebaki na Mkwasa.Kocha anayedai eti wachezaji wa timu pinzani wasijiangushe au ataondoka sio kocha. Huwezi ku dictate wachezaji wa timu zingine wafanye nini uwanjani.
ReplyDeleteUvumilivu hula mbivu.
ReplyDeleteAu hubakia na kilichooza.Akifungwa Leo atuachie timu yetu.GSM wamefanya makosa sana kushinikiza Mkwasa aondolewe aletwe kocha mpya.Viongozi hawana sauti tena kwani hata usajili unafanyiwa na GSM.
ReplyDelete