January 16, 2020


KUTOKANA na timu ya Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vanderbroeck kumrejesha ndani ya kikosi hicho mchezaji wao wa zamani, Shiza Kichuya, Saleh Jembe amekuwa na maswali matano ambayo anahitaji msaada kujibiwa.

Jembe amesema: "Kama umeelewa vizuri TUSAIDIANE.... Sijawahi kusema Shiza Kichuya ni mchezaji mbaya lakini nilikuwa najiuliza maswali kadhaa, kama una majibu TUSAIDIANE, ndio uanamichezo wenyewe... SIMBA KUMSAJILI KICHUYA NI KWA SABABU YA.... 1. Kuwahi Yanga wasimpate...
2. Siasa ya kupoza Sakata la bosi...
3. Kumsitiri kijana wao baada ya mambo kutoenda poa..
4. Usajili wa Simba una walakini kwa namba za pembeni
5. Kweli ni chaguo la Kocha au Nani anaamua... ....????

10 COMMENTS:

  1. Maswali ya kipumbavu haswa. Ungeanza na Kichuya ni mchezaji wa mpira?Kama Yanga wangemsajili ungeuuliza hayo maswali?Kweli kupooza sakata la bosi??Yanga wangemtaka???Unajiuliza haya maswali kwa usajili wa Simba tu??Yanga wakisajili unajiuliza?Kocha anashauriwa kwenye timu zote kwamba kuna mchezaji yupo available ni mchezaji wa aina gani.Yeye ndio anakuwa mwamuzi wa mwisho na benchi lake ya ufundi.

    ReplyDelete
  2. Kasajiliwa kuendeleza siasa za mpira wa Bongo usio na weledi ndani yake bali bora liende.. Binafsi siuoni umuhimu wake kwa Simba ya sasa yenye changamoto mbili tu. 1: Kukosa mshambuliaji wa kushirikiana na Kagere ambaye anaweza kusumbua mabeki na kuamua matokeo ndani ya dk 90.. 2: Kukosekana kwa Beki mahiri mwenye uwezo zaidi ya waliopo anayeweza kuwa tishio kwa washambuliaji wa VPL. Mimi nasema ikiwa tutaendelea kusajili kwa utaratibu huu UBINGWA wa CAF tutaendelea kuusikia kwa wenztu tu. Sijui tunakosea wap? Na sijui kwa nini Tanzania hatujifunzi au kwa sababu klabu zetu zimejaa wapiga madili tu. Binafsi pale Simba sikuona sababu ya kuwaleta wale Wabrazil watatu wenye uwezo sawa na wachezaji wetu. Ni maramia Tungeleta Striker mmoja hatari kariba ya kina Makusu na Beki mmoja tu. Sasa hebu angalia Haruna Shamte, Fraga, Tairone, Wilker, Kichuya hawana msaada wowote..

    ReplyDelete
  3. Ungeweka na swali la sita ...(6) None of my business

    ReplyDelete
  4. Maswali yenye kuchoma moyo, ila usajili huu ungekua na tija kama ungefanyika kabla ya usajili wa Luis kdg ningeelewa Simba inahitaji mtu wa kariba hiyo

    ReplyDelete
  5. Usajili wa Simba msimu huu una makandokando mengi sana. Haukuwa professional. Ikifika dirisha kubwa la usajili utasikia tumeacha wachezaji 15. Sasa sijui timu itatengeneza vipi faida ya kuuza wachezaji. Kichuya hana namba hata national team. Kama ni kumpa fadhila kwa mchango wake hapo nyumba, angepewa pesa ama majukumu mengine ndani ya club kama walivyo kina Mgosi. Na kama Simba wamefanya kuitibulia Yanga, basi wangeongea na timu nyingine let say Mtibwa wamchukue hata kama ni kuwasaidia kiasi cha malipo then akionesha kiwango kizuri msimu ujao wamsajili lakini si sasa.

    ReplyDelete
  6. Masuali uozo kabisa yaliyojaa unafiki.Nani asiemjua kichuya na ubora wake? Alipotangaziwa kichuya kwenye vyombo vya habari kuwa anakwenda Yanga,alipambwa na watu wote wa Yanga walisifu na kushinikiza asijiliwe haraka.Lakini Simba baada ya kumrejesha moja ya wachezaji wake waandamizi kabisa katika miaka hii ya karibuni kundini eti mtu ana hoji? Usajili wa babu Niyozima kwenda Yanga na Kinda kichuya Simba upi wa kuhoji?
    Lakini kama kuna hoja ya msingi ya kuhoji kwa mtu au muandishi makini kwanini usihoji Yanga kumleta kocha mpya wakati Mkwasa alikuwa anafanya vizuri tu na timu. Kwanini gharama za kumleta kocha mpya Yanga zisingetumika kuboresha maslahi ya Mkwasa na wachezaji? Hata hivyo kama kuna timu ilifanya usajili wa kipumabavu ligi kuu basi ni Yanga na wao wenyewe wanajua hilo. Maproo kadhaa walisajiliwa Yanga wamekuja kuchota pesa na kuondoka na kama ingekuwa Simba sijui ingukuwaje? Tuwache unafiki.

    ReplyDelete
  7. Hakuna maswali hapo ni unafiki na kuteseka tu!!!.

    ReplyDelete
  8. Maswali ya msingi hayo unasajili Kwa ajili ya kuwakomoa yanga huwezi kuendelea kisoka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic