AISHI
Manula, mlinda mlango wa Simba kwa sasa amekuwa gumzo kwa mashabiki kutokana na
kile wanachoeleza kwamba amefungwa mabao mengi ya kizembe kwa mashuti makali na
nje ya 18 kwa msimu huu wa 2019/20.
Kuna mengi
ambayo yapo kwenye timu ila linapokuja suala la matokeo mazuri hakuna ambaye
anamkubuka Manula ni mpaka pale atakapoboronga ndipo wengi wanamgeukia na kumtazama
kwa jicho la pili.
Kabla
sijafika mbali ndugu msomaji nikutakie kheri ya mwaka mpya 2020 kwa kuwa mambo
yanazidi kusonga mbele taratibu ni muda wa kujipanga na kuona kwamba kila mtu
anajua namna bora ya kutimiza malengo yake kwa wakati huu.
Kuna mengi
ambayo umeyapanga kwa mwaka 2020 ni vema ukamtanguliza Mungu na kufanya mambo
hayo kwa wakati ambao umejiwekea ili kutimiza ndoto zako ambazo unazifikiria
kwa muda wote wa masiha yako.
Mashabiki wa
soka wanapenda kuona matokeo chanya na yanapatikana ndani ya uwanja na sio nje
ya uwanja vita ya manenomaneno muda wake umekwishwa kwa sasa ni wakati mwingine
wa kuanza kufanya mambo bora kwa ajili ya kufikia mafanikio.
Turudi
kwenye mada ya leo ambapo nipo na mlinda mlango wa Simba, Manula ambaye
mashabiki wanamuona amechuja hana uwezo tena wa kukaa kwenye lango na badala
yake nafasi hiyo apewa Beno Kakolanya.
Ni ngumu
kumhukumu mlinda mlango huyo ambaye ni mlinda mlango namba moja ndani ya kikosi
cha Simba anapambana na rafikiye Beno Kakolanya alijiunga na Simba msimu wa
2017 akitokea klabu ya Azam FC.
Kwenye mechi
alizokaa langoni ambazo zimeikutanisha Simba na Yanga ni mechi sita mpaka sasa
ambazo ni sawa na dakika 540 na hakufungwa na Yanga zaidi ya kulazimisha sare
ama kushinda.
Kwenye jumla
ya mechi hizo sita Manula hajapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kupata sare
kwenye jumla ya mechi nne na kushinda mechi mbili.
Jumla ya
mabao ambayo ametunguliwa Manula ni mabao matatu pekee na mechi ya Jumamosi
inavunja rekodi kwa kufungwa mabao mengi ambayo ni mawili kwenye mechi moja
alizokutana na Yanga.
Matokeo ya
mechi ambazo Manula alikaa langoni zilikuwa namna hii:- 23/08/2017 hii ilikuwa
ni ngao ya jamii, Simba 0-0 Yanga, 28/10/2017 hii ilikuwa ni ya ligi, Yanga 1-1
Simba, 29/04/2018 ilikuwa ni ligi, Simba 1-0 Yanga,
30/09/2018 ilikuwa ya ligi,
Simba 0-0 Yanga, 16/02/2019 ilikuwa ni ya ligi, Simba 1-0 Yanga na Jumamosi,
Januari 4,2020 mechi yake ya sita na ilikuwa ya ligi Simba 2-2 Yanga.
Hapa
inaonyesha ni namna gani Manula amekuwa na uzoefu na mechi za Simba na Yanga
kwa muda ambao amekaa ndani ya Simba mpaka sasa.
Kwa msimu
huu Manula akiwa ndani ya Simba amekuwa chaguo la kwanza la makocha wote wawili
alianza akiwa chini ya Patrick Aussems ambaye alikaa langoni kwenye mechi zote
10 sawa na dakika 900 na alifungwa mabao matatu pekee.
Katika mabao
hayo matatu ni bao moja pekee alifungwa nje ya 18 ilikuwa mbele ya JKT
Tanzania, bao hilo lilifungwa na Edward Songo wakati Simba ikiibuka na ushindi
wa mabao 3-1 na mengine mawili yote alifungwa ndani ya 18.
Ikumbukwe
kuwa wakati Manula anacheza na Ruvu Shooting aliweza kuokoa aina ya mashuti ya
mbali na kuifanya ngome yake kuwa salama wakati wakiibuka na ushindi wa mabao
3-0 uwanja wa Uhuru.
Kwa bao lake
la pili la mbali alilofungwa msimu huu bado si wakati wa kumpigia kelele na
kuona kwamba hafai bado mpira ni mchezo wa makosa labda ndugu msomaji lile
shuti la Mapinduzi Balama ungekuwa wewe ndiye Manula ungefanyaje?
Tumpe sapoti
mtanzania mwenzetu na tujivunie vya kwetu, bado Tanzania ina walinda mlango
wachache kama ilivyo kwa washambuliaji, ila Manula ndugu yangu nawe unapaswa
ujifunze kupitia makosa.
Huu ni ujinga hauna hata mantiki ya kujadili.Hakuns kipa asiyefungwa.Waandishi uchwara wameanzisha glo tonic ili mradi wapate cha kujadili.Anafuungwa DeGea magoli ya mbali na hakuna anayeshangaa kwani ni sehemu ya mchezo.Akiokoa mashuti mbona hamna makala za kumsifia???
ReplyDeleteSahihi kabisa,kwa nini hawamsifii kwa kuandaa makala anavyofanya vizuri?..
Delete