January 10, 2020


KHLEFFIN Hamdoun, jembe jipya ndani ya Azam FC aliyesajiliwa kwa kadarasi ya miaka minne leo ataikosa mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba itakayochezwa Uwanja wa Gombani.
Arstica Cioaba, alivutiwa na uwezo wa kiungo huyo mshambuliaji wa Mlandege wakati timu yake ilipocheza mchezo wa robo fainali na kushinda bao 1-0 lililofungwa na Obrey Chirwa atashindwa kumtumia kiungo huyo kwa mujibu wa kanuni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mtendaji  Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, ‘ Popat’ amesema kuwa bado wapo chimbo kufanya usajili endapo Cioaba atahitaji ila hatamtumia kiungo wake mpya dhidi ya Simba.
“Ni kweli Cioaba anamkubali ila hataweza kumtumia dhidi ya Simba kwenye mechi yetu ya nusu fainali kwani tayari alishacheza akiwa Mlandege, na timu yake ilishatolewa hivyo atatumika kwenye mashindano  megine,” amesema Popat.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic