January 10, 2020


KUTOKANA na mashabiki wa Yanga kukasirika kitendo cha Yanga kupoteza mchezo wao wa nusu fainali kwenye Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar huku ikielezwa kuwa ni ujanja wa kuikimbia Simba uongozi wa Yanga umesema kuwa hakuna kitu kama hicho.

Yanga ilianza kufunga bao la kuongoza kwenye mchezo huo kupitika kwa Deus Kaseke jana Uwanja wa Amaan lilisawazishwa na Mtibwa Sugar dakika ya 90+2 na Shomari Kibwana na kupelekea kufungwa kwa penalti 4-2.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawaiogopi timu yoyote ni upepo tu haukuwa kwao jana.

"Tunacheza kwa malengo, wachezaji wamepambana kwa hali na mali mwisho wa siku tumefungwa usiku kutokana na makosa ya wachezaji wetu na bahati kuwa kwa Mtibwa Sugar.

"Upande wa penalti hazina mwenyewe tunarudi Bongo kujiaandaa na ligi, kuna mengi ya kufanya mashabiki watupe sapoti na hatujawakimbia Simba sisi," amesema.

Yanga wamerejea leo Bongo wakitokea Visiwani Zanzibar na wamewaacha wababe wao Mtibwa Sugar wakisubiri mshindi wa pili kati ya Azam ama Simba ili wacheze nao fainali, Januari 13.

10 COMMENTS:

  1. Endeleen kujifariji ila tambueni kila jambo lina mwanzo na mwisho wake,ukweli ni kwamba laiti mngepita jana basi mlikua muingie aibu ya mwaka maana mngefungwa magoli mengi sana ili mkatwe ngebe,mashsbiki wa yanga ni mapunguani kwasababu haiwezekani mnashangilia kupata sare kweli jamani inaingia akilin hio?acheni kujifariji ukweli utabaki pale pale kwamba yanga ni timu mbovu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ujinga wewe hiyo aibu mbona umeshindwa kuionesha taifa badala yake umemvalisha irizi kagere

      Delete
    2. Hivi zile 3-3 na goli la kichuya sijui watu awakushangilia mechi hizo au atukumbuki jamani

      Delete
    3. wewe ndio punguani usiejua soka bwege mkubwa weye.Kwa mtu yeyote anaejua soka bila kujali kuwa ni shabiki wa yanga au simba anatambua kuwa kilichotokea kwa yanga hata kingetokea kwa simba wangekuwa na furaha kama waliyonayo yanga.......issue sio kushangilia sare,issue ni fighting spirit iliyoonyeshwa na wachezaji wa yanga kutoka nyuma kwa goli mbili na kuchomoa ktk gemu kubwa na ngumu kama ile haikuwa kitu rahisi......ndio mana hata nyie mlipochomoa goli tatu kipindi kile mlishangilia sana,kwangu kushangilia kwa simba siku ile sikuona tatizo kwani naamini walistahili kushangilia kama ambavyo yanga walistahili mechi ya juzi.

      Delete
  2. Yaani u mwehu kweli kweli nyie simba mshukuru kupata droo kwa yanga

    ReplyDelete
  3. Wamekimbia haooooo kandambili haooooooo wangeona cha moto wamejuwa ndio wamekimbia

    ReplyDelete
  4. hirizi ni kufuatana na jicho na akili ya anyeiona hata cheini huitwa hirizi..Haiwezi ikawa hirizi halafu mwamuzi akaiokota akaipeleka kwa walioko benchi.Kikosi kilichochezeshwa Yanga jana kilimaanisha kuwa walikuwa hawataki kucheza fainali.Kadaka kipa namba tatu, Yondani kaingia kutoka benchi..Lamine aliendelea kukaa benchi na mastaa kama Haruna na Sibomana hawakuwepo.Isitoshe kaimu kocha pia hakuwepo..Sasa kama hizo sio dalili za kukimbia ni nini?Isitoshe mashabiki wengi wa Yanga walifurahi Yanga kuondolewa mashindanoni. ndiyo yele yale kwa wenye akili zao sale inaonekana lulu na kushangiliwa.Isitoshe Nungaz aliulizwa mapumziko ...hiki ni kikosi gani..Akajibu wana malengo yao wamekuja kushindana sio kushinda..Baadaye akasema mashindano haya madogo madogo yasije umiza wachezaji yahee..Angalia msije kosa kikombe mkiendelea kukumbia hata FA mtakimbia, na ngao ya jamii mtakimbia

    ReplyDelete
  5. Kambare hao wa jangwani bahati yao wanetukimbia hawana lolote

    ReplyDelete
  6. Kinachoshangiliwa ni comeback ndani ya dakika tatu, au wewe umesahau mliposhangilia sana sare ya 3-3 mlipotanguliwa kufungwa kisha mkarudisha, mbona hakuna aliyewatukana kama wewe unayetukana leo kwamba watu hawana akili? Jitambue au tukuelewe hujui usiku wala mchana?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic