UONGOZI wa Simba umesema kuwa kazi kubwa kwa kikosi chao kwa sasa itakuwa ni kupambana kwenye Kombe la Mapinduzi ili kufuta machungu ya kufungwa mabao 2 na watani zao Yanga ndani ya dakika saba.
Simba ilikuwa inaongoza kwenye mchezo wa Januari, 4, Uwanja wa Taifa ambao ulikuwa ni wa ligi ila Yanga walipindua meza kibabe kwa kufunga mabao mawili ndani ya dakika saba zilizowaondoa Simba mchezoni jumla na kufanya mchezo ukamilike kwa sare ya mabao 2-2.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ni wajibu kwa wachezji kupambana kulipa makosa yao waliyoyafanya uwanjani.
"Kwa sasa ni wakati wa kurudisha nguvu zetu na kupambana upya, wachezaji kosa mlilofanya mbele ya Yanga lisijirudie tena maana wenzetu kupata sare kwao ni ushindi," amesema.
Simba leo itarusha kete yake ya kwanza kwenye Kombe la Mapinduzi na itamenyana na Zimamoto uwanja wa Gombani.
Jamani angalieni msije mkafungwa na wala rojo
ReplyDelete