January 11, 2020


MANCHESTER United leo imewashushia kichapo timu ya Norwich City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa uwanja wa Old Trafford kwa kuichapa mabao 4-0.

Mabao ya United yalianza kupachikwa na mshambuliaji wao tegemeo, Marcus Rashford aliyepachika mabao mawili alianza dakika ya 22 na bao la pili alipachika dakika ya 52 kwa mkwaju wa penalti huku la tatu likipachikwa dakika ya 53 kupitia kwa Anthony Martial na msumari wa nne ulijazwa kimiani na Mason Greenwood dakika ya 78.

Ushindi huo unaifanya United ifikishe jumla ya pointi 34 ikiwa nafasi ya tano huku Norwich ikibaki na pointi zake 14 ikiwa inaburuza mkia nafasi ya 20.

Timu zote mbili zimecheza jumla ya mechi 22 za Ligi Kuu England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic