January 13, 2020


KOCHA Mkuu wa Yanga, LUC Eymael, raia wa Ubelgiji ambaye kwa sasa anamalizia hatua za awali za mkataba wake kabla ya kupewa majukumu rasmi amesema kuwa atafanya mambo makubwa ndani ya klabu hiyo.

Eymael anatarajiwa kutwaa mikoba ya Mwinyi Zahera ambaye alitimuliwa ndani ya klabu hiyo kutokana na kuboronga kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mechi za awali za ligi.

"Natambua kwamba aina ya timu niliyopewa ni ya aina gani, kila kitu kipo wazi kwani wachezaji nimewaona na nilikuwa ninawafuatilia sina mashaka katika hilo na maleng mkakubwa ni kuona timu inapata matokeo.

"Miongoni wa timu ambazo zinatajwa ndani ya Afrika ni Yanga kutokana na ukubwa wake sina wasiwasi, nina amini tutaanza na kuupigania ubingwa kwani ligi bado inaendela na hili linawekezana," amesema.


Mkataba wa Eymael unatajwa kuwa na vipengele vingi vigumu ambapo mojawapo ni kuhusu kurudisha ari na uwezo wa wachezaji pamoja na suala la kutwaa kombe la ligi ambalo lipo mkononi mwa Simba jambo linaloongeza vita ya moja kwa moja na wapnzani wao wakubwa Simba.

2 COMMENTS:

  1. Asitoe ahadi zitazomshinda kuzitimiza. Kutwaa ubingwa hasa mwaka huu asahau. Zahera alitowa ahadi na Jazba kama hizo na huku kuitendea Yanga makubwa alienziwa na kutukuzwa, aliifanyia Yanga kwa kuuweka mkono wake wazi pamoja na kuzungusha bakuli lakini yukowapi sasa. Kaondoshwa yeye pamoja na wachezaji aliowaleta aliposhindwa kutimiza ahadi zake

    ReplyDelete
  2. Hakuna vita yeyote mwaka huu Yanga anamaliza ligi katika nafasi ya tano.Subirini muone

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic